Make your own free website on Tripod.com

MACAVIRONDO

UKIMWI NA JAMII

Home | UKIMWI NA JAMII | BONGO EXPLOSION | ENGLISH MUSIC | SHUKRANI ZA DHATI

UKIMWI NA MAGONJWA YA ZINAA

Kirusi cha HIV  husababisha UKIMWI ambao sasa ni tatizo  la dunia. Urahisi wa safari za kimataifa  bila shaka umekuwa moja ya sababu kubwa za uambukizaji wa haraka wa HIV. Mwaka 1999 Shirika la Afya Duniani (WHO) ilikadiriwa kuwa watu wakubwa milioni 30 wana virusi vya HIV. Asilimia kubwa ya maambukizi haya yametokea katika nchi  zinazoendelea ambapo njia kuu ya kuambukizana ni kwa njia ya kujamiiana  kati ya mwanaume na mwanamke.
Wasafiri wanakadiriwa kuwa na uwezekano wa kuambukizwa virusi vya HIV mara 200 zaidi wakiwa nje ya nchi zao, kuliko wakiwa nchini kwao (nyumbani). 

      UKIMWI HUSABABISHWA NA NINI?

Ukimwi husababishwa na kirusi cha HIV. Kirusi hiki hushambulia kinga ya mwili na kuusababisha  ushindwe kupigana na magonjwa. Inaweza kuchukua miaka mingi kwa dalili za ugonjwa kujionyesha tokea unapoambukizwa. Hivyo mtu akionekana ya kwamba ana siha nzuri, siyo kwamba mtu huyu hajambukizwa  virusi  vya HIV.

Kirusi cha HIV hupatikana katika damu, shahawa na majimaji katika uke. Uambukizaji hutokea wakati kirusi kinapotokea katika mwili wa mtu aliyeambukizwa na kuingia katika mzunguko wa damu wa mtu mwingine.

 Hii hutokea kwa jinsi zifuatazo:

Kujamiiana kwa njia ya uke, njia ya haja kubwa, kutumia midomo, na kujamiiana bila kutumia mipira ya kiume (Kondomu)

Ngozi kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali kilicho na virusi vya ukimwi kama nyembe za kunyolea na kutahiria na sindano zinazotumika kuchorea miili, kutogea masiko, kuchanjia na kwa ajili ya huduma za afya katika nchi zinazoendelea.

Mgonjwa kupewa damu iliyoambukizwa na virusi vya HIV.

HUWEZI KUAMBUKIZWA KWA NJIA ZIFUATAZO

Mbu, kusalimiana, makalio ya vyoo vya kukalia,  kukohoa au kupiga chafya, kuogelea.

JINSI YA KUJIZUIA NA KIRUSI CHA ( HIV)

Kuacha kujamiiana ndiyo njia pekee ya kujizuia na magonjwa ya zinaa. Lakini kama unashindwa kujizuia kufanya mapenzi tumia kondomu  kwa usahihi. Kondomu inayotumiwa kwa usahihi  ndiyo njia pekee ya kujizuia dhidi ya HIV na magonjwa mengine ya zinaa ( isipokuwa warts, herpes na chawa).  Dawa za uzazi wa majira haziwezi kuzuia maambukizo ya UKIMWI

  UTOAJI WA DAMU

Baadhi ya nchi huhakikisha kwamba damu anayopewa mgonjwa, lazima ipimwe kama ina virusi vya HIV  lakini nchi nyingine huwa hazifanyi hivyo. Kama umeumia au unaumwa jitahidi kuepuka au kuahirisha kupewa damu isipokuwa kama ni lazima iwe hivyo. Kwa tukio la dharura, maji yanayochanganywa na damu (sterile plasma expanding fluid) yaweza kutumika badala ya damu kwa muda mfupi. Kama itabidi upewe damu,basi hakisha kuwa damu unayopewa imepimwa. Hakikisha kuwa una bima ya kusafiria itakayokusaidia kupata msaada wa matibabu popote pale ulimwenguni. 

MAGONJWA YA ZINAA

Hapa ni muhtasari tu wa baadhi ya magonjwa ya zinaa. Muda wa ugonjwa wa kukua ndani ya mwili ni muhimu kwani unaonyesha muda ulipoambukizwa hadi dalili zinapojitokeza.Wakati huu tendo la ndoa linapofanyika basi ugonjwa huu ndipo unapoenezwa kwa wengine

                                                                                                                                  

UGONJWA

MUDA

DALILI

Kisonono

Siku 2-7

Wanaume: Utoko mweupe (usaha) kutoka kwenye uume na maumivu makali wakati wa kukojoa. 
Kipimo: swabu na mkojo.

Wanawake: Mara nyingi hawana dalili.Wanaweza kuwa na usaha kwenye uke wenye harufu mbaya. 
Kipimo:
swabu

Klamidia

Siku 5-7

Wanaume: Utoko mwembamba usio na rangi na maumivu makali wakati wa kukojoa. 
Kipimo:
swabu au mkojo.

Wanawake: Mara nyingi hajikuna dalili au utoko kwenye uke
Kipimo
: Swabu

Kirusi cha herpes

Siku 2-12

Uvimbe/malengelenge kwenye uume au uke. Waweza kuambukizwa hata pasipo na malengelenge. 
Kipimo:Swabu

Umanjano (Hepatitis B)

Miezi 2-6

Dalili za ugonjwa wa manjano ( angalia kabrasha la (TMVS)
Kipimo; Damu

Kaswende

Siku 10-90

Dalili za mwanzo.Malengelenge yasiouma kwenye uume au uke. Dalili za pili.Ugonjwa kama mafua ukiambatana na upele.
Kipimo: damu

Kirusi cha duti

Miezi 10-20

Duti zinazoonekana au uke kuwasha.
Kipimo: Uchunguzi

       

Kwa kutumia mipira ya kiume (Kondomu) kila wakati wa tendo la ngono unapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa mmojawapo. 

UNAPOFIKA NYUMBANI

Kama ulifanya tendo la ngono wakati ukisafiri tafadhali unaporudi nyumbani kapime afya yako. Kama unadhani kwamba umeambukizwa virusi vya HIV basi usijamiiane au fanya tendo la ndoa kwa kutumia kinga utakaporudi nyumbani. Kumbuka kwamba vipimo vya damu kwa ajili ya virusi vya HIV huchukua miezi 3 kuthibitisha kama una virusi hivyo tokea ulipoambukizwa kwa mara ya kwanza na bado kuna uwezekano wa kuambikiza huu ugonjwa wakati huu. Kuzungumzia hili tatizo na mwenzi/mpenzi wako nyumbani na kuchukua tahadhari ya kujikinga laweza kuwa gumu, lakini ni muhimu kuzuia uenezaji wa huu  ugonjwa kwa watu

ILI USIKILIZE MIZIKI HII UNATAKIWA UDOWNLOAD TRELLIX PLAYER  
                              Powered By Trellix

*******MACAVIRONDO TUKO FITI MADUU SI MNATII*******